Wednesday, 25 May 2011

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA WARSHA YA SIKU MBILI KUHUSU UTAFITI YA VYUO VIKUU.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Warsha ya siku mbili kuhusu Utafiti, inayovishirikisha vyuo vikuu vya Dar es Salaam, Chuo cha Afya na Tiba Muhimbili na Chuo cha Ardhi. Warsha hiyo imeanza leo Mei 24 katika Hoteli ya White Sands na itamalizika kesho Mei 25.

Saturday, 21 May 2011

MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA SHUGHULI ZA MAZISHI YA SHEIKH YAHYA LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadiki (kulia) pamoja na baadhi ya viongozi,  wakiwa kwenye shughuli ya mazishi wa aliyekuwa mtabiri maarufu nchini, Sheikh Yahya, aliyefariki dunia jana jijini na anatarajia kuzikwa leo kwenye makaburi ya Tambaza.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA MAZIKO YA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA WAZEE WA CCM MKOA WA DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Athumani Hassan Mwinyimvua, aliyefariki dunia jana na kuzikwa jana Mei 20 kwenye Makaburi ya Karume Mwembechai.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA WAUGUZI MNAZI MMOJA DAR


  • Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akimkabidhi zawadi, Paul King’ara Muuguzi kutoka mkoani Mwanza wakati wa maadhimisho ya Sherehe za ya miaka 40 ya kuzaliwa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salam leo Mei 20.

Wednesday, 18 May 2011

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKAGUA UJENZI WA BARABARA YA MIZINGANI PEMBA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiangalia maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya Mizingani Wambaa, yenye urefu wa Kilometa 9.7 inayoendelea kujengwa, wakati alipotembelea na kukagua akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya Serikali kwenye mikoa ya Kaskazini na Kusini Pemba leo Mei 18. Aliyesimama upande wa kushoto wa Makamu wa Rais ni Ofisa msimamizi kutoka Wizara ya Mawasiliano na Miundombinu Zanzibar, Hamadi Baucha. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI SHULE YA MSINGI MJIMBINI KUSINI PEMBA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wanafunzi wa Shule ya Msingi Mjimbini iliyopo Mkoa wa Kusini Pemba, baada ya kuweka jiwe la Msingi katika shule hiyo leo Mei 18, akiwa katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ya Serikali kwenye mikoa ya Kaskazini na Kusini Pemba. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Tuesday, 17 May 2011

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ZIARANI MKOA WA KASKAZINI PEMBA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wanafunzi wa Shule ya Msingi Simai iliyopo Kijiji cha Wingwi Mapofu, Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, baada ya kuweka jiwe la msingi katika shule hiyo wakati akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo kwenye mikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba leo Mei 17.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL KATIKA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO PEMBA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuweka jiwe la Msingi katika   Ofisi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Tawi la Mtambile iliyopo Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba jana Mei 16, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya Maendeleo katika Mikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA WAZIRI WA UINGEREZA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Uingereza wa Masuala ya Kimataifa (Maendeleo), Stephen Obrien, wakati walipokutana kwa ajili ya mazungumzo katika moja ya ukumbi wa mikutano uliopo katika Ukumbi wa Plenary, ulipofanyika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo ya Nchi Masikini Duniani. Kushoto ni Msaidizi wa Waziri huyo, Greg Hicks (kulia) ni Balozi mdogo wa Tanzania nchini Italia, Salvator Mbilinyi na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mahadhi Juma Maalim.

Monday, 16 May 2011

MAKAMU WA RAIS DK BILAL AUNGURUMA ISTANBUL KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA KUHUSU MAENDELEO YA NCHI MASIKINI.

Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa mkutano wa Umoja wa Mataifa, ulioanza jijini Istanbul Uturuki Mei 9, ukitarajiwa kumalizika mei 13 mwaka huu. Mkutano huo unahusu Maendeleo ya nchi masikini.

Sunday, 8 May 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILALA AWASILI UTURUKI KUMWAKILISHA RAIS KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Msaidizi wa Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Modest Mero, baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Ataturk jijini Istambul jana Mei 7, 2011. Makamu wa Rais yuko nchini Uturuki kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika mkutano wa Umoja wa Matifa unaohusu maendeleo ya nchi maskini, Mkutano huo unaanza kesho na kumalizika Mei 13, 2011. Katikati ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA 'UNITED BANK OF AFRICA'

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Mkurugenzi  Mkuu wa  ‘United Bank Of Africa’ (UBA), Ajobola Abiola (katikati) wakati alipofika Ikulu Dar es Salaam jana ( Mei 5) kwa ajili ya mazungumzo. Kushoto ni Ofisa wa benki hiyo, Lilian Mboja.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA WAJUMBE WA KAMATI YA KUDUMU YA BARAZA LA WAWAKILISHI.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi (Hesabu za Serikali) Zanzibar, wakati walipofika Ikulu Dar es Salaam jana, kwa ajili ya mazungumzo na kumsalimia baada ya kumaliza mafunzo ya siku nne ya kamati hiyo kuhusu Usimamizi na Matumizi ya fedha za Serikali, yaliyomalizika hivi karibuni jijini Dar es salaam.

Monday, 2 May 2011

OFISI YA MAKAMU WA RAIS WASHIRIKI MEI MOSI DAR.

Baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakiandamana kuelekea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani "Mei Mosi" zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana na kuhudhuriwa na mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mecky Sadiki, . Sherehe hizo Kitaifa zilifanyika Mkoani Morogoro ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete.

Sunday, 1 May 2011

Makamu wa Rais audhuria hafla ya kuapishwa manaibu katibu wakuu.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akimpongeza Mwamini Juma Malemi, aliyekuwa msaidizi wa Makamu wa Rais (Maendeleo ya Jamii na Kero za Wananchi) katika Ofisi ya Makamu wa Rais ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakati wa hafla fupi ya kuwaapishwa Manaibu Katibu Wakuu iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam.

Serikali kulinda wanyamapori – Dk. Bilal


Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal ameihakikishia Taasisi ya kusaidia kuhifadhi wanyamapori Tanzania kuwa serikali itafanya kila jitihada ili kulinda wanyamapaori  nchini.
Akizungumza katika hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Taasisi hiyo katika hotel ya Moven Pick jijini Dar es salaam jana Dk. Bilal alisema hatua hiyo ya serikali inatokana na ukweli kwamba uhai wa wanayamapori ni suala linalohusu watu wote katika jamii.
Alisema  serikali itaanza mpango mkubwa na wa muda mrefu wa kupambana  na majangiri katika Hifadhi za Taifa na mbuga za wanyama na itakapobidi serikali iko tayari kutumia mbinu zote zilizopo kufanya operesheni maalum kulinda wanyamapori katika hifadhi hizo.
Alisema serikali pia inatarajia kutumia teknolojia ya kisasa katika kukabiliana na majangiri na hali kadhalika kutunga sheria kali ambazo zitakuwa na faini kubwa na pia kifungo cha muda mrefu kwa watu watakaobainika kuwa majangiri.
Makamu wa Rais alibainisha wazi kuwa tangu Taasisi hiyo ikutane kwa mara ya mwisho mwaka 2008 hifadhi za wanyamapori zimekuwa hatarini  kwa kuwa kiwango cha vitendo vya uhalifu kimeongezeka  na kusema tabia hiyo ya uhalifu haikubaliki kwani mbali ya kuhatarisha usalama wa wanyamapori lakini pia inatishia biashara ya utalii.
“Baadhi ya watafiti mashuhuri duniani wamekisia kuwa kiwango cha sasa cha ujangiri katika mbuga za wanyama, iwapo tembo hawatalindwa  dhidi ya majangiri wanaweza kupotea ndani ya miaka 10 ijayo. Kwa kweli hali hii inatukumbusha kazi kubwa iliyoko kwetu sote sisi,” alisema Makamu wa Rais.
Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Maliasili na Utalii Ezekiel Maige alielezea changamoto zilizopo ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa vitendo vya ujangiri katika maeneo ya hifadhi, upungufu wa magari na watumishi.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya shughuli hiyo J.K. Chande pamoja na kusisitiza serikali iweke sheria kali ya kuzuia majangiri pia alieleza kuwa Taasisi hiyo imefanikiwa kupata magari 15 aina ya Land Cruiser tangu ianzishwe mwaka 2001 kwa ajili ya kusaidia watumishi kuendesha shughuli zao.
Naye Mwakilishi wa Mtoto wa Mfalme wa Austria ambaye ni mweka hazina wa Taasisi hiyo Jacques Servais aliipongeza Taasisi ya kusaidia kuhifadhi wanyapori Tanzania kwa kufanikisha shughuli zake vyema tangu ilipozinduliwa mwaka 2001.
Hafla hiyo ambayo ilikuwa na lengo la kukusanya fedha ilihudhuriwa pia na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa ambaye ni mlezi wa Taasisi hiyo pamoja na mkewe Mama Anna Mkapa.


Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam
Jumapili – April 16, 2011