Wednesday, 27 July 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AAGA MWILI WA MAREHEMU PROFESA MUSHI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya marehemu Profesa, Samuel Mushi, aliyefariki wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. Shughuli za maziko na kuaga mwili wa marehemu zilifanyika kwenye Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo Julai 27, 2011. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima ya mwisho mbele ya jeneza lenye mwili ya Marehemu Profesa Samuel Mushi, wakati alipofika katika shughuli ya kuaga iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leo Julai 27, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, pamoja na baadhi ya viongozi wakiwa katika shughuli ya mazishi na kuaga mwili wa marehemu  Profesa Samuel Mushi, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo Julai 27, 2011.

Friday, 15 July 2011

JAKAYA KIKWETE NA DKT BILAL WAHUDHURIA NDOA YA YUSUPH KIKWETE BAGAMOYO LEO.

 Rais jakaya Kikwete na Makamu wake Dkt Mohammed Gharib Bilal, wakiongozana katika Uwanja vya Ikulu Ndogo Bagamoyo wakati walipofika kuhudhuria sherehe ya ndoa ya mdogo wake na rais Kikwete, Yusuph Kikwete, iliyofungwa leo mchana katika uwanja huo na kuhudhuriwa na mbalimbali pamoja na wake za viongozi.
Rais jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na mkewe Mama Salma Kikwete na Bwana na Bi Harusi.
Miraji Kikwete, naye hakuwa mbali katika kunasa matukio, hapa alikuwa akimpiga picha baba yake mdogo.


MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA RAIS WA MFUKO WA KUWAIT UKANDA WA AFRIKA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Rais wa Mfuko wa Kuwait Ukanda wa Afrika, Sheikh Fahdi  Mohammed Al-Shamri, wakati alipofika kumtembelea Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Julai 15 na kufanya naye mazungumzo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mfuko huo kwa upande wa Tanzania, Samy Mohammed.

Thursday, 14 July 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA MKUTANO MKUU WA TATU WA BARAZA LA WAKUU WA VYUO VIKUU HURIA AFRIKA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa mkuu wa tatu wa Baraza la Wakuu wa Vyuo Vikuu huria Afrika wa siku tatu kuhusu Elimu ya mafunzo ya Masafa uliofunguliwa lei Julai 13 kwenye Ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam na kuhudhuriwa na washiriki kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo wa siku 3, kuhusu mafunzo ya Elimu ya Masafa unaowashirikisha wakuu wa Vyuo Vikuu Huria kutoka nchi za Afrika, uliofunguliwa leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.

Monday, 11 July 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA KIGODA CHA KUMBUKUMBU YA MWL NYERERE.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kumbukumbu ya Kigoda cha Mwalimu Nyerere kinachohusika na masuala ya Mazingira na mabadiliko ya Tabianchi, kilichozinduliwa leo Julai 11, 2011 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kutangazwa kwa Mwenyekiti wa kwanza wa Kigoda hicho,  Prof. Pius Yanda. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Saturday, 9 July 2011

MAKAMU WA RAIS USO KWA USO NA MAALIM SEIF SABASABA BAADA YA KUZINDUA GS 1

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akikata utepe kuzindua rasmi huduma mpya ya Mfumo wa Utambuzi wa Bidhaa Tanzania, (Global Standard 1 ), wakati wa uzinduzi huo uliofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, julai 04
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, wakati walipokutana kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere katika Maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa leo Julai 04, 2011.

MABALOZI WA FINLAND NA UJERUMANI NCHINI TANZANIA WAMUAGA MAKAMU WA RAIS DKT BILAL

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Finland nchini Tanzania,  Juhan Toivonen , wakati alipofika ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam, Julai 04, 2011 kwa ajili ya kumuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake nchini. Picha na Muhidin Sufiani-OMR