Wednesday, 11 July 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA SINCHUAN HONGDA GROUP KUTOKA CHINA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti aliyeongozana na ujumbe Kutoka Hongda Group ya Beijing China, Quan Zhezhu, wakati ujumbe huo ulipofiak ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 11, 2012 kwa mazungumzo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Ujumbe Kutoka Hongda Group, Beijing China, wakati ujumbe huo ulipofiak ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 11, 2012 kwa mazungumzo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Monday, 9 July 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AMPOKEA MAKAMU WA RAIS WA AFRIKA YA KUSINI ALIYEFIKA NCHINI KWA ZIARA YA SIKU MBILI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na kuzunguma jambo na makamu wa Rais wa Afrika ya Kusini, Kgalema Motlanthe alipokuwa akimpokea Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpokea makamu wa Rais wa Afrika ya Kusini, Kgalema Motlanthe, aliyewasili nchini Julai 8, 2012 kwa ajili ya ziara ya siku mbili, ambapo atakuwa na mazungumzo na Makamu wa Rais Dkt. Bilal na kutatembelea Mazimbu mkoani Mororgoro. Picha na Muhidin Sufiani-OMR 

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL MGENI RASMI TUNZO ZA WASANII BORA 2012 WA MUZIKI WA ZANZIBAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya Heshima msanii mstaafu wa muziki wa Taarab, Mwanacha Hassan Kijole (65) wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa Tuzo hizo za Wasanii bora wa muziki wa Zanzibar wa mwaka 2012, zilizodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel.Hafla hiyo ilifanyika Julai 6, 2012 katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Uzini na Mkurugenzi wa redio ya Zenji Fm, Mohamed Seif Khatib (kushoto) ni Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Zantel, Zanzibar, Mohamed Baucha. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotub`a yake wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa Tuzo hizo za Wasanii bora wa muziki wa Zanzibar wa mwaka 2012,

Friday, 6 July 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AMWAKILISHA RAIS JAKAYA KIKWETE KUONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI MJINI DODOMA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimwakilisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete, kuongoza kikao cha  Baraza la Mawaziri, kilichofanyika leo mchana, julai 6, 2012 katika ukumbi wa TAMISEMI, mjini Dodoma. Picha na Muhidin Sufiani-OMR