Wednesday, 31 August 2011

MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI SWALA YA EID EL FITR MNAZI MMOJA DAR.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa pili kulia) Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (kulia), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Ibrahim Lipumba (kushoto), wakiwa katika swala ya Eid El-Fitr, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo, Agosti 31. Picha na Muhidin Sufiani.

Monday, 29 August 2011

RAIS DKT. JAKAYA NA MAKAMU DKT. BILAL WAFUTURU PAMOJA NA WANANCHI DAR.

Rais Dkt. Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Meck Dadick, wakiomba dua kwa pamoja baada ya kupata futari iliyoandaliwa na mwenyeji wao Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika makazi yake Oysterbay jijini jana.

Friday, 5 August 2011

MAKAMU WA RASI DKT BILAL AKUTANA NA MBUNGE WA WAWI HAMAD RASHI, MJINI DODOMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Wawi (CUF) Hamad Rashid, wakati  walipokutana nyumbani  kwa  Makamu mjini Dodoma hivi karibuni. Katikati ni Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd. Picha na Muhidin Sufiani.

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ATEMBELEA MABANDA MAADHIMISHO YA PILI YA NANE NANE MJINI DODOMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja ya Tela la Trekta linalotengenezwa nchini, wakati wa  wakati wa hafla ya maadhimisho ya  mwaka wa pili wa utekelezaji wa Kaulimbiu ya Kilimo Kwanza Agosti 03, 2011 ikiwa ni sehemu ya maonyesho ya Nane Nane zinazoendelea katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi funguo ya Trekta la kilimo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Teresia Huvisa, kwa ajili ya matumizi ya kilimo, wakati wa hafla ya maadhimisho ya  mwaka wa pili wa utekelezaji wa Kaulimbiu ya Kilimo Kwanza Agosti 03, 2011 ikiwa ni sehemu ya maonyesho ya  Nane Nane zinazoendelea katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.