Wednesday, 30 November 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGA MKUTANO WA NCHI ZA MAZIWA MAKUU BUJUMBURA BURUNDI.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Tanzania, nchini Burundi, Dkt. James Mwasi, baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Golf  kwa ajili ya kufunga Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu, uliokuwa ukijadili Uendelezwaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika, uliomalizika jana Novemba 29, Bujumbura Burundi.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Makamu wa Rais wa Burundi, Therence Sinunguruza, wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Golf  kwa ajili ya kufunga Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu, uliokuwa ukijadili Uendelezwaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika, uliomalizika jana Novemba 29, Bujumbura Burundi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya kufunga Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu, uliokuwa ukijadili Uendelezwaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika, uliomalizika jana Novemba 29, kwenye Ukumbi wa Golf, Bujumbura Burundi.

Monday, 28 November 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA SIKU YA VIONGOZI WA TAKUKURU-TANGA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Viongozi wa Takukuru Mkoani Tanga Novemba 28. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Takukuru, Edward Hosea (kushoto) ni Waziri wa Ofisi ya Rais-Utawala Bora, Mathias Chikawe.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Takukuru, Edward Hosea, wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Viongozi wa Takukuru, uliofanyika Mkoani Tanga leo Novemba 28. Kushoto ni Waziri wa Ofisi ya Rais- Utawala Bora, Mathias Chikawe.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Takukuru.

Saturday, 26 November 2011

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, ahudhuria Mahafali ya 23 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia Viongozi na wahitimu katika ngazi mbalimbali kwenye mahafali ya 23 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika tarehe 26 Nov 2011, Bungo Kibaha Dar es salaam.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA TAMASHA LA SIKU YA MTANZANIA LA WATU WA JAMII YA RUKWA NA KATAVI, JIJINI DAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati akimpa maelezo kuhusu kinywaji cha kienyeji Pombe ya Chimpumu inayotumiwa na Kabila la watu wa Rukwa, wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Siku ya Utamaduni wa Mtanzania iliyowasilishwa na Kabila la Jamii za Mikoa ya Rukwa na Katavi, lililofanyika kwenye Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam jana Novemba 25.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoka ndani ya nyumba ya asili ya watu wa Kabila la Wafipa, wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Siku ya Utamaduni wa Mtanzania 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakitembelea mabanda ya maonyesho na kujionea Bidhaa za Vyakula vya asili vinavyotumiwa zaidi na watu wa Mikoya ya Rukwa na Katavi,Makamu wa Rais akikabidhiwa mkuki kama ilivyo katika mila za watu wa Rukwa na Katavi.

Saturday, 19 November 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA UMOJA WA WABUNGE WA TANZANIA WA KUPAMBANA NA UKIMWI MJINI DODOMA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya picha Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge wa Tanzania wa kupambana na Ukimwi (TAPAC), Lediana Mng’ong’o, kwa kuwa mstari wa mbele katika kusimamia umoja huo, wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Umoja huo tangu ulipoanzishwa. Uzinduzi huo ulifanyika kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma, Novemba 18, 2011
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiinua Mshumaa juu baada ya kuuwasha ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Umoja wa Wabunge wa Tanzania wa kupambana na Ukimwi (TAPAC), uliofanyika kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma, Novemba 18. Katikati ni Spika wa Bunge, Anne Makinda na Mwenyekiti wa Umoja huo, Lediana Mg’ong’o wakishangilia uzinduzi huo.

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA MDAHALO WA NAFASI YA UMUHIMU WA KATIBA KTK MAISHA YA WATANZANIA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua Mdahalo wa Nafasi ya Umuhimu wa Katiba katika Maisha ya Watanzania, uliofunguliwa Novemba 17, katika Jumba la Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS APOKEA MADAI YA WANANCHI KUHUSU MABADILIKO YA TABIA NCHI.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa Kongamano la Msafara wa kuelekea katika mkutano wa mabadfiliko ya Tabia Nchi unaotarajia kufanyika Durban Afrika ya Kusini mwezi ujao. Kongamano hilo limefanyika Novemba 15, 2011 kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Thursday, 10 November 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AONGOZA MAJADILIANO YA MKUTANO WA UWEKEZAJI WA CHAKULA NA KILIMO.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa Mkutano wa Uwekezaji wa Chakula na Kilimo, ulioanza leo Novemba 10, 2011  kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa Uwekezaji wa Chakula na kilimo, baada ya kuongoza mkutano huo.

Wednesday, 9 November 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ASAINI TAMKO LA VIONGOZI WA DINI KUHUSU MABADILIKO YA TABIA NCHI.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini tamko la Viongozi wa dini kuhusu mabadiliko ya Tabia Nchi, wakati wa Tamasha la Vijana la ‘Tunaimani kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi’ lililofanyika kwenye Viwanja vya Don Bosco Upanga jijini Dar es Salaam leo Novemba 9, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya vijana hao kuelekea Durban kushiriki katika Mkutano wa 17 wa Mabadiliko ya Tabia nchi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu, nchini Afrika ya Kusini. Kushoto ni Askofu Mkuu wa Jimbo la Tabora na Mwenyekiti wa Viongozi wa Dini Nchini, Askofu Paul Ruzoka. 
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa Tamasha la wakati wa Tamasha la Vijana la ‘Tunaimani kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi’.

Friday, 4 November 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA MKUTANO WA MAWAZIRI WA WIZARA ZA MAENDELEO YA WANAWAKE NA WATOTO WA NCHI ZA MAZIWA MAKUU, JIJINI ARUSHA.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Wanawake na Watoto Zanzibar, Zainab Omar, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Arusha, kwa ajili ya kufungua rasmi Mkutano wa Mawaziri wa Wizara za Maendeleo ya Wanawake na Watoto, wa Nchi za Maziwa makuu, ulioanza leo Novemba 4, katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mkuu wa Mkoa Arusha, Mulongo Magesa, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba na Balozi Liberata Mulamula, wakati akiingia kwenye Ukumbi wa Mikutano wa AICC.

Thursday, 3 November 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA MKURUGENZI WA MAZINGIRA, MAANDALIZI YA MKUTANO WA DURBAN.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Julius Ningu, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Novemba 3, 2011, kuzungumzia maandalizi ya Mkutano wa 17 wa Nchi zilizoridhia mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya Tabia nchi unaotarajia kuanza mwishoni mwa mwezi huu  Durban Afrika ya Kusini. Kushoto ni, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulikia mabadiliko ya Tabianchi, Richard Muyungi.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA WAKURUGENZI WA TPDC NA TIC.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mafuta nchini (TPDC), Yona Killagane, wakati walipokutana kwa mazungumzo Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam Novemba 2, 2011. Kushoto ni Mkurugenzi Masoko na Uwekezaji wa Shirika hilo, Dismas Fuko.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Ujumbe wa Kituo cha Uwekezaji  Tanzania (TIC) wakati walipofika ofisini kwake jijini Ikulu Dar es Salaam, Novemba 2, 2011.