Monday, 19 March 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA MAADHIMISHO YA WIKI YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI (VETA) KITAIFA MKOANI TANGA.

 Makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia viatu na kusikiliza maelezo kuhsu utengenezaji wa bidhaa hiyo kutoka kwa Deogratias John (kushoto)  wa Chuo cha Waleavu cha Usariva Moshi, wakati akitembelea katika mabanda ya maonyesho alipozindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, yaliyoanza leo Machi 19 Kitaifa mkoani Tanga. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Kapteni Mstaafu, Chiku Galawa. Wa pili (kushoto) ni Mkurugenzi wa VETA, Mhandisi. Zebadiah Moshi. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha VETA mkoa wa Tanga, baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Tangamano, Kwa ajili ya kuzindua maadhimisho ya Wiki ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, yaliyoanza leo Machi 19 Kitaifa mkoani Tanga.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua mashine ya king’ola kuzindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Mkoani Tanga.

Sunday, 18 March 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA UJUMBE WA KUJITATHMINI KI-UTAWALA BORA KATIKA AFRIKA ‘AFRICAN PEER REVIEW MECHANISM’ (APRAM)


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na ujumbe wa Kujitathmini Ki-Utawala Bora katika Afrika ‘African Peer Review Mechanism’ (APRM) wakati ujumbe huo ulipomtembelea Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Machi 16, 2012 kwa ajili ya mazungumzo.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipiga picha ya pamoja kwa kumbukumbu pamoja na Wajumbe wa  Kujitathmini Ki-Utawala Bora katika Afrika ‘African Peer Review Mechanism’ (APRM)  baada kumaliza mazungumzo na Ujumbe huo uliofika Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Machi 16, 2012 kwa ajili ya mazungumzo.

Tuesday, 6 March 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA MKUTANO WA SIKU MBILI WA KIMATAIFA WA KUPEANA UZOEFU KUHUSU MALIPO YANAYOTOKA KWA WAFADHILI KWA UFANISI.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt.Haji Mponda, baada ya kufungua mkutano wa siku mbili wa Kimataifa wa kujadili na kubadilishana mawazo kuhusu ufadhili wa mkiradi yenye ufanisi katika nchi saba za Afrika Mashariki, ulioanza leo Machi 6, 2012 jijini Dar es Salaam.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa siku wenye lengo la kujadili na kubadilishana mawazo kuhusu ufadhili wa mkiradi yenye ufanisi katika nchi saba za Afrika Mashariki, ulioanza leo Machi 6, 2012 jijini Dar es Salaam.

Thursday, 1 March 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AMALIZA ZIARA YAKE YA MKOA WA IRINGA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Iwawa baada ya kuzungumza nao wakati akimaliza ziara yake ya Wilaya ya Makete Mkoa wa Iringa jana Februari 28, 2012.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti cha kumiliki hisa katika Benki ya Wananchi (NJOCOBA), Zela Edward, bada ya kuzindua rasmi benki hiyo iliyopo Wilaya ya Njombe mkoa wa Iringa jana Februari 28, 2012.

Makau wa Rai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkurugenzi wa Nishati katika Kiwanda cha SAO Hill, Roselyne Mariki, wakati  alipowasili katika kiwanda hicho jana Februari 28, 2012 kwa ajili ya kuzindua mashine mpya nay a kisasa ya kuchana mbao.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya silaha ya jadi ya kabila la Wahehe (Mkuki) kutoka kwa Mjukuu wa Chifu Mkwawa, Ignas Muyinga, baada ya kumaliza kuzindua kituo cha afya na kuwahutubia wananchi wa Kijiji cha Lungemba, Wilaya ya Mafinga mkoa wa Iringa, jana Februari 28, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wananchi wa Kijiji cha Lungemba baada ya kuwahutubia wananchi hao, Wilaya ya Mafinga mkoa wa Iringa, jana Februari 28, 2012.