Wednesday 25 April 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AADHIMISHA SIKU YA MALARIA DUNIANI NA KUZINDUA RIPOTI YA MAFANIKIO A UTEKELEZAJI WA MIKAKATI YA MALARIA TANZANIA BARA.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisoma hotuba yake wakati wa Kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Malaria
Duniani, zilizofanyika leo Aprili 25, 2012 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es
Salaam. Katika sherehe hizo pia Makamu wa Rais alizindua Ripoti ya utekelezaji wa mikakati ya malaria, Tanzania Bara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akikata utepe, kuzindua Ripoti ya Mafanikio ya Utekelezaji wa Mikakati ya Malaria kwa
upande wa Tanzania Bara, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Malaria
Duniani zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo Aprili 25,
Katikati ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Haji Mponda (wapili kushoto) ni Kaimu
 mkuu wa Wilaya za Kinondoni, Temeke na Ilala, Jordan Lugimbana.
 

Monday 23 April 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI MAZISHI YA BRIGEDIA GENERAL MSTAAFU ADAM MWAKANJUKI UNGUJA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka mchanga katika kaburi la Brigedia General Mstaafu, Adam Mwakanjuki, wakati wa maziko yake yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Mwanakwerekwe mjini Unguja, Aprili 22, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, Shimbo, akiweka mchanga katika kaburi la Brigedia General Mstaafu, Adam Mwakanjuki.
 Mke wa Marehemu Brigedia General mstaafu, Adam Mwakanjuki, Bi. Ikupa Mwakanjuki, akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu mumuwe, wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kwenye makaburi ya Mwanakwerekwe mjini Unguja.

Wednesday 18 April 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA DINI LA WAISLAMU NA WAKRISTO JIJINI DAR.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa dini alipowasili kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam,kwa ajili ya kufungua Kongamano la Dini la Waislam na Wakristo, lililoanza leo Aprili 18, 2012.

 Baadhi ya Viongozi wa Dini wakifuatilia kwa makini Hotuba ya Mgeni Rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipofika kufungua rasmi Kongamano la Dini la Waislam na Wakristo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Kongamano .


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya Viongozi wa Dini.

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA MAONYESHO YA 7 YA ELIMU YA JUU YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu na Utafiti yaliyoanza Aprili 18, 2012 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwalimu Simon Shayo, wakati alipotembelea katika Banda la Chuo Kikuu cha DUCE cha jijini Dar es Salaam, alipofika kuzindua maonyesho ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu na Utafiti yaliyoanza leo Aprili 18, 2012 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee. Kushoto ni Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Chuo hicho, Abdul Njaid.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Akisikiliza maelezo kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Ardhi, Prof. Mangisen Kaseva, wakati alipotembelea katika Banda la Chuo hicho baada ya kuzindua maonyesho ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu na Utafiti yaliyoanza leo Aprili 18, 2012 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee. Kulia ni Ofisa Utawala  wa Chuo hicho, Rosemary Bundara. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na baadhi ya wafanyakazi wa TCU.

Tuesday 17 April 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ASAINI KITABU CHA KUMBUKUMBU CHA KIFO CHA ALIYEKUWA RAIS WA MALAWI, DKT. BINGU WA MUTHARIKA LEO.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maomboleo ya aliyekuwa Rais wa Malawi, Dkt. Bingu wa Mutharika, katika Ofisi za Ubalozi wa Malawi nchini, zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam, Aprili 17, 2012. Kulia ni Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Flossie Asekanao Gomile-Chidyaonga. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA 26 MWAKA WA PAMOJA KWA WADAU WA SAYANSI ULIOANDALIWA NA TAASISI YA TAIFA YA UTAFITI WA MAGONJWA YA BINADAMU (NIMR)

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Mwele Malecela (watatu kushoto) kuhusu maonyesho ya wanasayansi yaliyoandaliwa  na Taasisi ya Taifa ya Utafiti ya magonjwa ya Binadam (NIMR) wakati alipofika kufungua mkutano wa 26 wa mwaka wa wadau wa sayansi ulioanza Aprili 16, jijini Arusha. Wa pili (kushoto) ni mke wa Makamu, Mama Zakhia Bilal na (kulia) ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Haji Mponda.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa 26 wa mwaka wa Wadau wa Sayansi  ulioandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)

Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na wadau wa Sayansi waliohudhuria mkutano huo wa 26 wa mwaka wa Wadau wa Sayansi jijini Arusha.

Monday 16 April 2012

MAKAMU WA RAIS AZINDUA BENKI YA ACB JIJINI ARUSHA LEO, AWEKA JIWE LA MSINGI.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wakati alipokuwa akizindua rasmi jengo la Benki ya ACB jijini Arusha leo Aprili 16, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya ACB ya jijini Arusha, Dkt. Jonas Kipokola, wakifunua kitambaa kuashiria kuweka Jiwe la Msingi katika Benki hiyo mpya wakati Makamu alipofika jijini humo kuizindua rasmi leo Aprili 16, 2012. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Benki ya ACB Tawi la Arusha, Anna Kavishe, kuhusu utendaji wa kazi na ramani ya jengo jipya la benki hiyo, baada ya kuizindua rasmi leo Aprili 16, 2012, jijini Arusha. Wapili (kulia) ni Mke wa Makamu Mama Zakhia Bilal na Kulia kwa Makamu ni Mwenyekiti wa Bodi wa Benki hiyo, Jonas Kipokola.

Friday 13 April 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA CHUO CHA UFUNDI STADI CHA VETA MKOA WA LINDI

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal na Balozi wa Korea nchini, Young-Hoon Kim, wakikata utepe kwa pamoja kuashiria
uzinduzi rasmi wa Chuo kipya cha Ufundi Stadi cha VETA kilichojengwa Mkoa wa Lindi.
Uzinduzi huo ulifanyika jana Aprili 10, 2012. Kulia ni Mkurugenzi wa VETA, Zebadia Moshi.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akibonyeza 'Alam', kuashiria uzinduzi rasmi wa Chuo kipya cha Ufundi Stadi cha VETA
kilichojengwa Mkoa wa Lindi.
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA baada ya
kuzindua rasmi chuo hicho
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Ghariub Bilal,
akisikiliza maelezo kuhusu jinsi ya ufundishaji wanafunzi kwa kutumia mtambo wa kufua
Umeme, kutoka kwa Mwalimu wa Umeme Veta, Majolo Mwigole, wakati Makamu alipofika kuzindua chuo hicho

Sunday 1 April 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA JENGO LA OFISI ZA TAWI LA CCM MWANAKWEREKWE B, MKOA WA MJINI MAGHARIBI UNGUJA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi kwenye Jengo la Ofisi za Tawi la CCM Mwanakwerekwe B, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja jana, Machi 30, 2012. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mjini Magharib, Mohammed Yussuf.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia jambo na Mbunge wa Jimbo la Mwanakwerekwe, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha (kushoto) na mmoja kati ya wazee wa eneo hilo ambaye ni kati ya wazee waliokuwa na kucheza ‘Chandim’ pamoja.