Wednesday 26 October 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AHUDHURIA MKUTANO WA MAWASILIANO WA KIMATAIFA GENEVA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika ufunguzi wa mkutano wa Mawasiliano wa Kimataifa, uliofanyika Oktoba 25, Geneva Switzerland, ambapo Tanzania ilikuwa ni moja kati ya nchi zilizoshiriki katika maonyesho ya mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza katika mkutano wa Mawasiliano wa Kimataifa.

Saturday 22 October 2011

MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI MAADHIMISHO YA KILELE CHA MIAKA 50 YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa Kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tangu kilipoanzishwa mwaka 1961. Sherehe hizo zimefanyika leo Oktoba 22, katika Ukumbi wa Nkrumah  Chuo Kikuu jijini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Kitivo cha Sheria, baada ya kutoa tuzo kwa baadhi ya wanafunzi wa zamani wa Taaluma ya Sheria waliosoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Wednesday 19 October 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AHUDHURIA SHEREHE ZA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA SAMORA MACHEL-MAPUTO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,mkewe Mama Zakhia Bilal na Mama Maria Nyerere,wakiwa pamoja na baadhi ya Marais wa nchi za Afrika wakati walipohudhuria katika maadhimisho ya Kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Muasisi na Rais wa Msumbiji, Samora Machel, zilizofanyika leo Oktoba 19, mjini Maputo Msumbiji.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na aliyekuwa mke wa Rais wa zamani wa Msumbiji, Mama Grace Machel, wakati walipokutana na katika viwanja vya Mozambique Heroes Square, kwenye sherehe za maadhimisho ya Kumbukumbu ya kifo cha muasisi wa nchi hiyo, Samora Machel, zilizofanyika leo Oktoba 19, mjini Maputo. Kulia kwa Makamu ni Mama Zakhia Bilal na (katikati) ni Rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma.

Friday 14 October 2011

MAKAMU WA RAISI KATIKA SHUGHULI YA KUWASHWA KWA MWENGE WA UHURU.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Mwenge wa uhuru kiongozi wa mbia za mwenge huo mwaka 2011 2012 Mtumwa Rashid Halfan kutoka mkoa wa kaskazini Unguja, kwa ajili ya kuanza mbio za kukimbiza katika mikoa yote ua Tanzania baada ya kuuwasha rasmi leo katika kijiji cha Butiama Mkoani Mara.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka shada la mauwa kwenye Kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwalim Julius Nyerere baada ya misa maalum ya kumkumbuka muasisi huyo Taifa la Tanzania iliyofanyika leo kijijini kwake Mwitongo Butiama.

Thursday 13 October 2011

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA MAKAO YA WATOTO YATIMA, MSONGOLA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuzindua jiwe la msingi la Kituo cha kulelea watoto Yatima na waishio katika mazingira magumu cha Full Gospel Children’s Home, kilichopo Msongola Wilaya ya Ilala Dar es Salaam. Hafla hiyo ya uzinduzi wa kituo hicho ulifanyika leo Oktoba 13, 2011
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Kituo cha kulelea watoto Yatima cha Full Gospel Children’s Home
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika Picha ya pamoja na Viongozi wa Kituo cha kulelea watoto Yatima cha Full Gospel Children’s Home, kilichopo Msongola wilaya ya Ilala, baada ya kuzinduliwa kwa kituo hicho.

Wednesday 12 October 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ATOA POLE MSIBA WA MTOTO WA MWAPACHU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika Kitabu cha maombolezo cha Harith Mwapachu, ambaye ni mtoto wa Balozi Juma Mwapachu, aliyefariki dunia jana Oktoba 11, 2011.Kulia ni Balozi Juma Mwapachu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha (CHADEMA) Freeman Mbowe, wakati walipokutana katika msiba wa mtoto wa Balozi Juma Mwapachu.