Tuesday, 14 June 2011

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO NEW YORK, ASISITIZA KUZINGATIA MAONI KUHUSU KATIBA.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Watanzania waishio New York na Vitongoji vyake, wakati alipokutana nao kwa ajili ya mazungumzo jana Juni 12, 2011. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA BAN KI MOON, AUNGURUMA JIJINI NEW YORK KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA KUHUSU UGONJWA WA UKIMWI

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Ban Ki Moon, wakati alipokutana naye kwa mazungumzo ofisini kwake jijini New York, Juni 8, 2011 baada ya kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ugonjwa wa Ukimwi.

Saturday, 4 June 2011

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA MATAIFA YA TROPIKI YALIYO UKANDA WENYE MISITU MIKUBWA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili katika viwanja vya Bunge la Jamhuri ya watu wa Kongo jijini Brazzaville, jana Ijumaa, Juni 3, 2011 kuhudhuria Mkutano wa 3 wa Nchi za Tropiki zilizo katika ukanda wenye misitu mikubwa na mvua nyingi. Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka katika nchi zaidi ya 30 zilizo katika ukanda huo, mataifa yaliyoalikwa sambamba na mashirika ya Kimataifa yanayoshughulika na masuala ya mazingira. Picha na ofisi ya Makamu wa Rais.