Saturday 26 November 2011

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA TAMASHA LA SIKU YA MTANZANIA LA WATU WA JAMII YA RUKWA NA KATAVI, JIJINI DAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati akimpa maelezo kuhusu kinywaji cha kienyeji Pombe ya Chimpumu inayotumiwa na Kabila la watu wa Rukwa, wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Siku ya Utamaduni wa Mtanzania iliyowasilishwa na Kabila la Jamii za Mikoa ya Rukwa na Katavi, lililofanyika kwenye Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam jana Novemba 25.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoka ndani ya nyumba ya asili ya watu wa Kabila la Wafipa, wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Siku ya Utamaduni wa Mtanzania 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakitembelea mabanda ya maonyesho na kujionea Bidhaa za Vyakula vya asili vinavyotumiwa zaidi na watu wa Mikoya ya Rukwa na Katavi,Makamu wa Rais akikabidhiwa mkuki kama ilivyo katika mila za watu wa Rukwa na Katavi.

No comments:

Post a Comment