Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Wanawake na Watoto Zanzibar, Zainab Omar, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Arusha, kwa ajili ya kufungua rasmi Mkutano wa Mawaziri wa Wizara za Maendeleo ya Wanawake na Watoto, wa Nchi za Maziwa makuu, ulioanza leo Novemba 4, katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mkuu wa Mkoa Arusha, Mulongo Magesa, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba na Balozi Liberata Mulamula, wakati akiingia kwenye Ukumbi wa Mikutano wa AICC.
No comments:
Post a Comment