Wednesday, 9 November 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ASAINI TAMKO LA VIONGOZI WA DINI KUHUSU MABADILIKO YA TABIA NCHI.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini tamko la Viongozi wa dini kuhusu mabadiliko ya Tabia Nchi, wakati wa Tamasha la Vijana la ‘Tunaimani kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi’ lililofanyika kwenye Viwanja vya Don Bosco Upanga jijini Dar es Salaam leo Novemba 9, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya vijana hao kuelekea Durban kushiriki katika Mkutano wa 17 wa Mabadiliko ya Tabia nchi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu, nchini Afrika ya Kusini. Kushoto ni Askofu Mkuu wa Jimbo la Tabora na Mwenyekiti wa Viongozi wa Dini Nchini, Askofu Paul Ruzoka. 
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa Tamasha la wakati wa Tamasha la Vijana la ‘Tunaimani kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi’.

No comments:

Post a Comment