Saturday, 19 November 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA UMOJA WA WABUNGE WA TANZANIA WA KUPAMBANA NA UKIMWI MJINI DODOMA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya picha Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge wa Tanzania wa kupambana na Ukimwi (TAPAC), Lediana Mng’ong’o, kwa kuwa mstari wa mbele katika kusimamia umoja huo, wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Umoja huo tangu ulipoanzishwa. Uzinduzi huo ulifanyika kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma, Novemba 18, 2011
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiinua Mshumaa juu baada ya kuuwasha ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Umoja wa Wabunge wa Tanzania wa kupambana na Ukimwi (TAPAC), uliofanyika kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma, Novemba 18. Katikati ni Spika wa Bunge, Anne Makinda na Mwenyekiti wa Umoja huo, Lediana Mg’ong’o wakishangilia uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment