Wednesday 21 September 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL MGENI RASMI UTIAJI SAINI MKATABA WA MIRADI YA MAKAA YA MAWE YA MCHUCHUMA NA CHUMA CHA LIGANGA BAINA YA NDC NA KAMPUNI YA CHINA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akishuhudia zoezi la utiaji saini na kubadilishana  mkataba wa miradi ya Makaa ya mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya China, wakati Mwenyekiti wa Bodi ya NDC, Christant Mzindakaya na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, Liu Canglong, wakisainiana mkataba huo katika ukumbi wa mlimani City jijini Dar es Salaam, leo Septemba 21, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye utiaji saini mkataba wa miradi ya Makaa ya Mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya nchini China, uliofanyika kwenye ukumbu wa Mlimani City Dar es Salaam

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akishuhudia zoezi la utiaji saini mkataba wa miradi ya Makaa ya mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya China, wakati Mwenyekiti wa Bodi ya NDC, Christant Mzindakaya na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, Liu Canglong, wakisainiana mkataba huo.

No comments:

Post a Comment