Monday 26 September 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO SWEDEN.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wenyeji wake baada ya kuwasili kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Gillet Clarion iliyopo Uppsala Sweden jana, kwa ajili ya kuzungumza na Watanzania waishio nchini humo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Watanzania, waishio nchini Sweden wakati alipokutana nao jana Septemba 25, katika Ukumbi wa Hoteli ya Gillet Clarion iliyopo Uppsala Sweden. Kuliani ni Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Muhammed Mwinyi Mzale.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha pa kumbukumbu pamoja na baadhi ya watanzania, waishio nchini Sweden, baada ya kumaliza mazungumzo nao.

No comments:

Post a Comment