Tuesday 13 September 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA JENGO LA MIHADHARA LA DUCE M.158 ZACHANGWA KUSAIDIA UJENZI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Jengo la Mihadhara na kuchangisha fedha za ujenzi wa Maabara ya Shule ya Sekondari Chang’ombe, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika katika Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCE jijini Dar es Salaam leo Septemba 13, 2011. Kusho ni mwakilishi wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha UDSM, Prof. Yunus Mgaya na (kulia) ni Mkuu wa Chuo hicho Kikuu Kishiriki cha DUCE, Prof. Salome Misana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuzindua Jiwe la Msingi la Jengo la Mihadhara la Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCE, uzinduzi uliambatana na uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Maabala ya Shule ya Sekondari Chang’ombe, ambapo katika zoezi hilo la uchangishaji fedha Makamu alichangia Sh. Milioni 10, na kufanya jumla ya michango kufikia Sh. Milioni 158.

No comments:

Post a Comment