Tuesday 27 September 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AUNGURUMA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA IDARA YA SAYANSI ZA KIMATAIFA SWEDEN.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa mhadhara na kuelezea uzoefu wa Tanzania kuhusu changamoto za sayansi wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Idara ya Sayansi za Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Uppsala kilichopo Sweden. Mhadhara huo uliambatana na safari ya Makamu wa Rais katika maabara mbalimbali zilizopo chuoni hapo jana Sept. 26, 2011.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Uppsala Sweden, Bo Sundavist (katikati) na Mkurugenzi, Romain Murenzi, wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ua Idara ya Sayansi za Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Uppsala kilichopo nchini Sweden. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Prof. Mohamed Hassan (kushoto) Prof. Jean-Piere Ezin (wapili kushoto) na Prof. Mohamed Elton, baada ya kumalizika kwa Mhadhara

No comments:

Post a Comment