Thursday, 29 September 2011

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA WAZIRI WA MAENDELEO NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA WA SWEDEN.

Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akichangia katika kongamano la lililoandaliwa na Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa wa Sweden, Gunilla Carlsson, kuhusu nafasi ya uhusiano wa Tanzania na Sweden, lililofanyika jijini Stockholm Sweden.
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya picha yenye Taswara ya mjini wa Zanzibar, Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa wa Sweden, Gunilla Carlsson, wakati Makamu alipofika Ofisini kwa waziri huyo jijini Stockholm Sweden kwa mazungumzo

Tuesday, 27 September 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AUNGURUMA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA IDARA YA SAYANSI ZA KIMATAIFA SWEDEN.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa mhadhara na kuelezea uzoefu wa Tanzania kuhusu changamoto za sayansi wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Idara ya Sayansi za Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Uppsala kilichopo Sweden. Mhadhara huo uliambatana na safari ya Makamu wa Rais katika maabara mbalimbali zilizopo chuoni hapo jana Sept. 26, 2011.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Uppsala Sweden, Bo Sundavist (katikati) na Mkurugenzi, Romain Murenzi, wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ua Idara ya Sayansi za Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Uppsala kilichopo nchini Sweden. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Prof. Mohamed Hassan (kushoto) Prof. Jean-Piere Ezin (wapili kushoto) na Prof. Mohamed Elton, baada ya kumalizika kwa Mhadhara

Monday, 26 September 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO SWEDEN.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wenyeji wake baada ya kuwasili kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Gillet Clarion iliyopo Uppsala Sweden jana, kwa ajili ya kuzungumza na Watanzania waishio nchini humo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Watanzania, waishio nchini Sweden wakati alipokutana nao jana Septemba 25, katika Ukumbi wa Hoteli ya Gillet Clarion iliyopo Uppsala Sweden. Kuliani ni Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Muhammed Mwinyi Mzale.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha pa kumbukumbu pamoja na baadhi ya watanzania, waishio nchini Sweden, baada ya kumaliza mazungumzo nao.

Saturday, 24 September 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA KITABU CHA ‘QUANTUM MACHENICS’ CHA PROF, JOHN KONDORO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Kitabu cha ‘Quantum Mechanics’ kilichotungwa na Professa. John Kondoro, wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika Septemba 22, katika Ukumbi wa Chuo cha DIT, jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (wapili kushoto) Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Charles Kitwanga (wapili kulia) Prof. John Kondoro mtunzi wa kitabu cha ‘Quantum Machenics’ na Makamu Mkuu wa Chuo cha DIT, Prof. Christian Nyahumwa (kushoto) wote kwa pamoja wakifurahia baada ya Makamu kuzindua kitabu hicho, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo cha DIT, jijini Dar es Salaam. 

Wednesday, 21 September 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL MGENI RASMI UTIAJI SAINI MKATABA WA MIRADI YA MAKAA YA MAWE YA MCHUCHUMA NA CHUMA CHA LIGANGA BAINA YA NDC NA KAMPUNI YA CHINA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akishuhudia zoezi la utiaji saini na kubadilishana  mkataba wa miradi ya Makaa ya mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya China, wakati Mwenyekiti wa Bodi ya NDC, Christant Mzindakaya na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, Liu Canglong, wakisainiana mkataba huo katika ukumbi wa mlimani City jijini Dar es Salaam, leo Septemba 21, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye utiaji saini mkataba wa miradi ya Makaa ya Mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya nchini China, uliofanyika kwenye ukumbu wa Mlimani City Dar es Salaam

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akishuhudia zoezi la utiaji saini mkataba wa miradi ya Makaa ya mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya China, wakati Mwenyekiti wa Bodi ya NDC, Christant Mzindakaya na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, Liu Canglong, wakisainiana mkataba huo.

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Dickson Maimu, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Septemba 21 kwa ajili ya mazungumzo kuhusu maendeleo ya maandalizi ya zoezi hilo la vitambulisho vya Taifa. Katikati ni Ofisa habari wa NIDA, Rose Mdami.

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA MWAKILISHI WA KATIBU WA UMOJA WA MATAIFA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Marta Santos Pais, Mwakilishi maalum wa Katibu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na harakati za kutokomeza unyanyasaji wa watoto, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo kuhusu ripoti ya unyanyasaji wa watoto inayohusu hali ya Tanzania na inayotarajiwa kuwasilishwa rasmi hivi karibuni (Jumanne, Septemba 2011.

Tuesday, 13 September 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA JENGO LA MIHADHARA LA DUCE M.158 ZACHANGWA KUSAIDIA UJENZI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Jengo la Mihadhara na kuchangisha fedha za ujenzi wa Maabara ya Shule ya Sekondari Chang’ombe, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika katika Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCE jijini Dar es Salaam leo Septemba 13, 2011. Kusho ni mwakilishi wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha UDSM, Prof. Yunus Mgaya na (kulia) ni Mkuu wa Chuo hicho Kikuu Kishiriki cha DUCE, Prof. Salome Misana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuzindua Jiwe la Msingi la Jengo la Mihadhara la Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCE, uzinduzi uliambatana na uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Maabala ya Shule ya Sekondari Chang’ombe, ambapo katika zoezi hilo la uchangishaji fedha Makamu alichangia Sh. Milioni 10, na kufanya jumla ya michango kufikia Sh. Milioni 158.

MAKAMU WA RAIS AWAFARIJI WALIOPOTELEWA NA NDUGU KATIKA AJALI YA MELI ZANZIBAR.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na viongozi na wakazi wa Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja, wakati alipofika katika eneo hilo kwa ajili ya kuwafariji wakazi hao waliopatwa na matatizo pamoja na kukagua shughuli za uokoaji zinazoendelea.

Friday, 9 September 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AAGANA NA MABALOZI WA VATICAN NA JAPAN, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Hiroshi Nakagawa, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Septemba 9, 2011 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Vatican nchini Tanzania, Askofu Mkuu Joseph Chennoth, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Septemba 9, 2011 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake nchini. Balozi Chennoth amekaa nchini miaka sita.

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA 20 WA MAGAVANA WA AFRIKA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba katika ufunguzi wa mkutano wa 20 wa Bodi ya Magavana wa Afrika (ACBF), uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha leo Septemba 08, 2011

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano wa 20 wa Magavana wa Afrika, baada ya kufungua mkutano huo.