Wednesday, 18 April 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA MAONYESHO YA 7 YA ELIMU YA JUU YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu na Utafiti yaliyoanza Aprili 18, 2012 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwalimu Simon Shayo, wakati alipotembelea katika Banda la Chuo Kikuu cha DUCE cha jijini Dar es Salaam, alipofika kuzindua maonyesho ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu na Utafiti yaliyoanza leo Aprili 18, 2012 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee. Kushoto ni Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Chuo hicho, Abdul Njaid.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Akisikiliza maelezo kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Ardhi, Prof. Mangisen Kaseva, wakati alipotembelea katika Banda la Chuo hicho baada ya kuzindua maonyesho ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu na Utafiti yaliyoanza leo Aprili 18, 2012 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee. Kulia ni Ofisa Utawala  wa Chuo hicho, Rosemary Bundara. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na baadhi ya wafanyakazi wa TCU.

No comments:

Post a Comment