Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Mwele Malecela (watatu kushoto) kuhusu maonyesho ya wanasayansi yaliyoandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti ya magonjwa ya Binadam (NIMR) wakati alipofika kufungua mkutano wa 26 wa mwaka wa wadau wa sayansi ulioanza Aprili 16, jijini Arusha. Wa pili (kushoto) ni mke wa Makamu, Mama Zakhia Bilal na (kulia) ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Haji Mponda.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa 26 wa mwaka wa Wadau wa Sayansi ulioandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)
Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na wadau wa Sayansi waliohudhuria mkutano huo wa 26 wa mwaka wa Wadau wa Sayansi jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment