Monday, 16 April 2012

MAKAMU WA RAIS AZINDUA BENKI YA ACB JIJINI ARUSHA LEO, AWEKA JIWE LA MSINGI.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wakati alipokuwa akizindua rasmi jengo la Benki ya ACB jijini Arusha leo Aprili 16, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya ACB ya jijini Arusha, Dkt. Jonas Kipokola, wakifunua kitambaa kuashiria kuweka Jiwe la Msingi katika Benki hiyo mpya wakati Makamu alipofika jijini humo kuizindua rasmi leo Aprili 16, 2012. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Benki ya ACB Tawi la Arusha, Anna Kavishe, kuhusu utendaji wa kazi na ramani ya jengo jipya la benki hiyo, baada ya kuizindua rasmi leo Aprili 16, 2012, jijini Arusha. Wapili (kulia) ni Mke wa Makamu Mama Zakhia Bilal na Kulia kwa Makamu ni Mwenyekiti wa Bodi wa Benki hiyo, Jonas Kipokola.

No comments:

Post a Comment