Sunday, 1 April 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA JENGO LA OFISI ZA TAWI LA CCM MWANAKWEREKWE B, MKOA WA MJINI MAGHARIBI UNGUJA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi kwenye Jengo la Ofisi za Tawi la CCM Mwanakwerekwe B, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja jana, Machi 30, 2012. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mjini Magharib, Mohammed Yussuf.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia jambo na Mbunge wa Jimbo la Mwanakwerekwe, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha (kushoto) na mmoja kati ya wazee wa eneo hilo ambaye ni kati ya wazee waliokuwa na kucheza ‘Chandim’ pamoja.

Monday, 19 March 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA MAADHIMISHO YA WIKI YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI (VETA) KITAIFA MKOANI TANGA.

 Makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia viatu na kusikiliza maelezo kuhsu utengenezaji wa bidhaa hiyo kutoka kwa Deogratias John (kushoto)  wa Chuo cha Waleavu cha Usariva Moshi, wakati akitembelea katika mabanda ya maonyesho alipozindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, yaliyoanza leo Machi 19 Kitaifa mkoani Tanga. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Kapteni Mstaafu, Chiku Galawa. Wa pili (kushoto) ni Mkurugenzi wa VETA, Mhandisi. Zebadiah Moshi. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha VETA mkoa wa Tanga, baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Tangamano, Kwa ajili ya kuzindua maadhimisho ya Wiki ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, yaliyoanza leo Machi 19 Kitaifa mkoani Tanga.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua mashine ya king’ola kuzindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Mkoani Tanga.

Sunday, 18 March 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA UJUMBE WA KUJITATHMINI KI-UTAWALA BORA KATIKA AFRIKA ‘AFRICAN PEER REVIEW MECHANISM’ (APRAM)


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na ujumbe wa Kujitathmini Ki-Utawala Bora katika Afrika ‘African Peer Review Mechanism’ (APRM) wakati ujumbe huo ulipomtembelea Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Machi 16, 2012 kwa ajili ya mazungumzo.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipiga picha ya pamoja kwa kumbukumbu pamoja na Wajumbe wa  Kujitathmini Ki-Utawala Bora katika Afrika ‘African Peer Review Mechanism’ (APRM)  baada kumaliza mazungumzo na Ujumbe huo uliofika Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Machi 16, 2012 kwa ajili ya mazungumzo.

Tuesday, 6 March 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA MKUTANO WA SIKU MBILI WA KIMATAIFA WA KUPEANA UZOEFU KUHUSU MALIPO YANAYOTOKA KWA WAFADHILI KWA UFANISI.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt.Haji Mponda, baada ya kufungua mkutano wa siku mbili wa Kimataifa wa kujadili na kubadilishana mawazo kuhusu ufadhili wa mkiradi yenye ufanisi katika nchi saba za Afrika Mashariki, ulioanza leo Machi 6, 2012 jijini Dar es Salaam.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa siku wenye lengo la kujadili na kubadilishana mawazo kuhusu ufadhili wa mkiradi yenye ufanisi katika nchi saba za Afrika Mashariki, ulioanza leo Machi 6, 2012 jijini Dar es Salaam.

Thursday, 1 March 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AMALIZA ZIARA YAKE YA MKOA WA IRINGA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Iwawa baada ya kuzungumza nao wakati akimaliza ziara yake ya Wilaya ya Makete Mkoa wa Iringa jana Februari 28, 2012.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti cha kumiliki hisa katika Benki ya Wananchi (NJOCOBA), Zela Edward, bada ya kuzindua rasmi benki hiyo iliyopo Wilaya ya Njombe mkoa wa Iringa jana Februari 28, 2012.

Makau wa Rai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkurugenzi wa Nishati katika Kiwanda cha SAO Hill, Roselyne Mariki, wakati  alipowasili katika kiwanda hicho jana Februari 28, 2012 kwa ajili ya kuzindua mashine mpya nay a kisasa ya kuchana mbao.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya silaha ya jadi ya kabila la Wahehe (Mkuki) kutoka kwa Mjukuu wa Chifu Mkwawa, Ignas Muyinga, baada ya kumaliza kuzindua kituo cha afya na kuwahutubia wananchi wa Kijiji cha Lungemba, Wilaya ya Mafinga mkoa wa Iringa, jana Februari 28, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wananchi wa Kijiji cha Lungemba baada ya kuwahutubia wananchi hao, Wilaya ya Mafinga mkoa wa Iringa, jana Februari 28, 2012.

Tuesday, 28 February 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AANZA ZIARA YA MKOA WA IRINGA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka jiwe la Msingi katika Soko lililojengwa kwa nguvu za wananchi la Mfumbi, baada ya kuwasili Wilaya ya Makete kuanza ziara ya siku tatu mkoani humo jana Februari 27, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
 Makamu wa Rai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa matunda wa kumbukumbu katika eneo la Chuo cha VETA cha Wilayani Makete mkoa wa Iringa, baada ya kuweka jiwe la msingi katika chuo hicho ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya mkoani Iringa jana Februari 27, 2012.

Saturday, 25 February 2012

MAKAMU WA RAIS AZINDUA SOKO LA TUNDUMA LILILOUNGUA MOTO MWAKA JANA BAADA YA KUKARABATIWA UPYA.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Soko la Tunduma lililofanyiwa ukarabati baada ya kuungua moto mwaka jana, wakati akianza rasmi ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Mbeya jana Februari 24, 2012. Kushoto ni Mkewe Mama Asha Bilal, (kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro na (kulia kwake) ni Mbunge wa Mbozi Magharibi David Silinde.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye eneo la Soko la Tunduma jana Februari 24, 2012, kwa ajili ya kuzindua soko hilo baada ya kukamilika kwa ukarabati wake kufuatia moto ulioteketeza soko hilo mwaka jana. Makamu wa Rais amewasili mkoani Mbeya jana kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Tunduma wakati alipofika eneo hilo kwa ajili ya kuzindua Soko la Tunduma baada ya kukamilika kwa ukarabati kufuatia soko hilo kuungua moto mwaka jana.