Monday 19 March 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA MAADHIMISHO YA WIKI YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI (VETA) KITAIFA MKOANI TANGA.

 Makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia viatu na kusikiliza maelezo kuhsu utengenezaji wa bidhaa hiyo kutoka kwa Deogratias John (kushoto)  wa Chuo cha Waleavu cha Usariva Moshi, wakati akitembelea katika mabanda ya maonyesho alipozindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, yaliyoanza leo Machi 19 Kitaifa mkoani Tanga. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Kapteni Mstaafu, Chiku Galawa. Wa pili (kushoto) ni Mkurugenzi wa VETA, Mhandisi. Zebadiah Moshi. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha VETA mkoa wa Tanga, baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Tangamano, Kwa ajili ya kuzindua maadhimisho ya Wiki ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, yaliyoanza leo Machi 19 Kitaifa mkoani Tanga.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua mashine ya king’ola kuzindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Mkoani Tanga.

No comments:

Post a Comment