Monday 9 July 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL MGENI RASMI TUNZO ZA WASANII BORA 2012 WA MUZIKI WA ZANZIBAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya Heshima msanii mstaafu wa muziki wa Taarab, Mwanacha Hassan Kijole (65) wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa Tuzo hizo za Wasanii bora wa muziki wa Zanzibar wa mwaka 2012, zilizodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel.Hafla hiyo ilifanyika Julai 6, 2012 katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Uzini na Mkurugenzi wa redio ya Zenji Fm, Mohamed Seif Khatib (kushoto) ni Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Zantel, Zanzibar, Mohamed Baucha. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotub`a yake wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa Tuzo hizo za Wasanii bora wa muziki wa Zanzibar wa mwaka 2012,

No comments:

Post a Comment