Thursday, 17 May 2012

MAWAZIRI WA ARDHI, MAZINGIRA WATOA TAARIFA YA ZOEZI LA BOMOA BOMOA NYUMBA ZA UFUKWENI NCHINI.

Kuelekea mchakato utakaoanza hivi karibuni wa kuendesha zoezi la bomoa bomoa ya nyumba ambazo zimejengwa kimakosa bila kufuata sheria na kanuni za ujenzi na makazi, na hivyo basi ujenzi huo holela katika maeneo ya ufukweni kumesababisha uharibifu wa mazingira ya fukwe hizo. Mawaziri wenye dhamana ambao ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Terezya Huvisa, wamekutana na Makamu wa Rais, Mhe. Gharib Bilal ili kujadili juu ya mwenendo na namna ya kulikabili zoezi hilo.

      Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, amekutana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Terezya Huvisa, kwa mazungumzo na kupokea taarifa ya zoezi la Bomoa bomoa  nyumba zilizojengwa maeneo ya Ufukweni, ambalo linatarajia kuanza hivi karibuni.

 Mazungumzo hayo yalifanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu Dar es Salaam leo Mei 17, 2012. Katika picha kutoka (kushoto) ni Katibu wa Wizara ya Ardhi, Veldiana Mashingia, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka (kulia) ni Mkurugenzi wa Mazingira, Dkt. Julius Ningu na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa, baada ya mazungumzo hayo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment