MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA TAASISI YA WAKURUGENZI TANZANIA (IoDT)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IODT), wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika leo Mei 10, 2012 kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo upande wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Mussa Juma (wa pili kulia) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora) George Mkuchika na (kushoto) ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Pius Maneno. Picha na Muhidin Sufiani
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya Tuzo ya Heshima, Ibrahim Mohamed Kaduma, kwa kuwa Mwanachama wa Heshima wa Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IODT)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma Hotuba yake wakati akizindua rasmi Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na Viongozi na baadhi ya wadau walioshiriki katika hafla hiyo ya uzinduzi, baada ya kuzindua rasmi Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT) uliofanyika leo Mei 10 kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment