Wednesday, 23 May 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA KITABU CHA ‘CHECKLIST OF TANZANIAN SPECIES.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha ‘Checklist Of Tanzanian Species’, iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Mei 22, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Baadhi ya wadau waliohudhulia uzinduzi huo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha Kitabu cha ‘Checklist Of Tanzanian Species’ baada ya  kukizindua rasmi kitabu hicho.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza Meneja wa Shirika la TANBIF Node, Hulda Gideon, wakati alipotembelea sehemu ya maonyesho yaliyoandaliwa na Shirika hilo kwenye uzinduzi wa Kitabu cha ‘Checklist Of Tanzanian Species’

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika Picha ya pamoja na wadau waliohudhuria uzinduzi huo.

Monday, 21 May 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA MKUTANO WA SIKU NNE WA KUBADILISHANA UZOEFU BAINA YA SERIKALI YA TANZANIA NA CHINA KUHUSU MAFUNZO YA ULINZI.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal. Akisoma hotuba yake wakati akifungua mkutano wa siku nne wa kubadilishana uzoefu baina ya Serikali ya Tanzania na China, kuhusu mafunzo ya Ulinzi. Ufunguzi huo umefanyika leo Mei 21, 2012 katika Chuo kipya cha Jeshi National Defence College (NDC) kilichojengwa na Wachina eneo la Kunduchi jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Liutenant General wa Jeshi la Bangladesh, M F Akbar, baada ya kufungua rasmi mkutano.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Meja General Charles Lawrence Makakala.

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakati Makamu wa Rais Dkt Bilal, akifungua mkutano huo leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo mara baada ya kuufungua rasmi leo.

Thursday, 17 May 2012

MAWAZIRI WA ARDHI, MAZINGIRA WATOA TAARIFA YA ZOEZI LA BOMOA BOMOA NYUMBA ZA UFUKWENI NCHINI.

Kuelekea mchakato utakaoanza hivi karibuni wa kuendesha zoezi la bomoa bomoa ya nyumba ambazo zimejengwa kimakosa bila kufuata sheria na kanuni za ujenzi na makazi, na hivyo basi ujenzi huo holela katika maeneo ya ufukweni kumesababisha uharibifu wa mazingira ya fukwe hizo. Mawaziri wenye dhamana ambao ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Terezya Huvisa, wamekutana na Makamu wa Rais, Mhe. Gharib Bilal ili kujadili juu ya mwenendo na namna ya kulikabili zoezi hilo.

      Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, amekutana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Terezya Huvisa, kwa mazungumzo na kupokea taarifa ya zoezi la Bomoa bomoa  nyumba zilizojengwa maeneo ya Ufukweni, ambalo linatarajia kuanza hivi karibuni.

 Mazungumzo hayo yalifanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu Dar es Salaam leo Mei 17, 2012. Katika picha kutoka (kushoto) ni Katibu wa Wizara ya Ardhi, Veldiana Mashingia, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka (kulia) ni Mkurugenzi wa Mazingira, Dkt. Julius Ningu na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa, baada ya mazungumzo hayo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Friday, 11 May 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATOA MSAADA KWA VITUO VIWILI VYA WATOTO YATIMA DAR.

 Msaidizi wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, eneo la Makaazi,
Peleleja Masesa (kushoto) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula, Mkurugenzi Mkuu wa
Kituo cha kulelea Watoto Yatima cha Orphanasi Trust Fund Msongola, Deusdelit Mitauto, kwa
niaba ya Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal. Makabidhiano hayo yalifanyika jana jijini Dar es salaam.

Thursday, 10 May 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA TAASISI YA WAKURUGENZI TANZANIA (IoDT)

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IODT),  wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika leo Mei 10, 2012 kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo upande wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Mussa Juma (wa pili kulia) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora) George Mkuchika na (kushoto) ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Pius Maneno. Picha na Muhidin Sufiani

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya Tuzo ya Heshima, Ibrahim Mohamed Kaduma,  kwa kuwa Mwanachama wa Heshima wa Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IODT)

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma Hotuba yake wakati akizindua rasmi Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na Viongozi  na baadhi ya wadau walioshiriki katika hafla hiyo ya uzinduzi, baada ya kuzindua rasmi Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT) uliofanyika leo Mei 10 kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Tuesday, 8 May 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA JUKWAA LA UCHUMI WA KIJANI LA SIKU 3 MKOANI IRINGA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akizindua rasmi Jukwaa la Uchumi wa Kijani, litakaloendelea kwa siku tatu Mkoani Iringa. Uzinduzi huo umefanyika leo Mei 8, 2012, katika Ukumbi wa Shule ya Msingi Mtakatifu Dominic Savio, mkoani Iringa. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Shule ya Msingi Mtakatifu Dominic Savio, baada ya kuzindua rasmi Jukwaa la Uchumi wa Kijani.