Saturday, 25 February 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AMALIZA ZIARA YAKE YA MKOA WA RUKWA NA KATAVI KWA KUZINDUA KAMPENI YA SUMBAWANGA NG’ARA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikabidhi vifaa vya kufanyia usafi kwa viongozi wa kampuni za kufanya usafi katika mitaa ya mjini Sumbawanga, wakati akizindua kampeni ya Sumbawanga Ng’ara  kwa ajili ya kudumisha usafi wa mazingira, ikiwa ni siku yake ya mwisho ya ziara yake katika mkoa wa Katavi na Rukwa jana Februari 24, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
  Makamu wa Rai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Kampeni ya Sumbawanga Ng’ara yenye lengo la kudumisha usafi wa mazingira mjini Sumbawanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mama Asha Bilal (kushoto kwake) na Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Rukwa, Eng. Stella Manyanya (kulia kwake) na baadhi ya viongozi wa mji wa Sumbawanga, mbele ya Sanamu la Sumbawanga Ng’ara baada ya kuzindua kampeni hiyo jana Februari 24, 2012.

No comments:

Post a Comment