Monday 30 January 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA MASHAMBA YA MPUNGA YA KOROGWE, AWEKA JIWE LA MSINGI JENGO LA UKUMBI NA OFISI YA HALMASHAURI YA KOROGWE.

Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Madiwani wa Kata za Wilayani Korogwe, alipowasili eneo hilo kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi katika Jengo la Ukumbi na Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, wakati akiwa katika ziara yake ya Wilaya ya Korogwe mkoa wa Tanga, Januari 27, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi katika jengo jipya la Ukumbi na Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, wakati alipokuwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya Wilaya ya Korogwe mkoa wa Tanga

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Viongozi wa Wilaya ya Korogwe, wakikagua jengo la Ukumbi na Ofisi ya Halmashauri ya Korogwe 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wakulima wa Mpunga kuhusu kilimo hicho cha umwagiliaji wakati alipotembelea na kukagua mashamba ya Skim Mamlaka ya mji wa Mombo

 Makamu wa Rais wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akikagua mitaro ya maji yanayotumika kumwagilia mashamba ya mpunga ya Skim.

No comments:

Post a Comment