Friday, 2 December 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA BARABARA YA NELSON MANDELA TEMEKE JIJINI DAR.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKt. Mohammed Gharib Bilal na Kaimu Balozi wa Umoja wa Ulaya, Enrico Strampeli, wakifunua kitambaa kwa pamoja ikiwa ni sehemu ya Ufunguzi wa  jiwe la Msingi la Barabara, wakati wa ufunguzi wa Barabara hiyo ya Mandela uliofanyika jijini Dar es Salaam, Desemba 2.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu baada ya kufungua rasmi Barabara ya Nelson Mandela, uliofanyika Desemba 2, Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Kaimu Balozi wa Umoja wa Ulaya, Enrico Strampeli , wakikata upete kwa pamoja ikiwa ni ishara ya ufunguzi rasmi wa Barabara ya Nelson Mandela, uliofanyika leo Desemba 2, Temeke Jijini Dar es Salaam. Kulia kwa Makamu ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli na (kulia) kwa Balozi ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadick.

No comments:

Post a Comment