Monday, 12 December 2011

MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI HAFLA YA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA WA KIISLAM WA 1433.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waumini na viongozi wa Jumuiya ya Kiislamu ya Istiqaama, baada ya kumalizilika kwa halfa hiyo Desemba 12.
Add caption
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba wakati wa halfa ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kiislam iliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiqaama Tanzania Tawi la Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika Desemba 11, 2011 katika Ukumbi wa Karimjee jijini.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakati akiondoka kwenye Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam, Desemba 12, baada ya kumaliza shughuli ya hafla ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kiislam iliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiqaama Tawi la Dar es Salaam.

Wednesday, 7 December 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AHUDHURIA MKUTANO WA 17 WA MABADILIKO YA TABIANCHI DURBAN-AFRIKA YA KUSINI.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akizungumza wakati wa mkutano wa majadiliano wa Viongozi wakuu 194 wa nchi wanachama  wa Itifaki wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya Tabianchi, juu ya kupunguza uzalishaji wa gesijoto Duniani kabla ya kuanza kwa mkutano mkuu wa 17 wa umoja huo uliofanyika jana Desemba 6 mjini Durban, Afrika ya Kusini.

Saturday, 3 December 2011

MAKAMU WA RAIS ATOA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA YA MAREHEMU DAVID WAKATI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Mtangazaji wa TBC, David Wakati, alipofika nyumbani kwa marehemu huyo  Oysterbay jijini Dar es Salaam jana Desemba 2, kwa ajili ya kutoa mkono wa pole. Marehemu Wakati alifariki juzi jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Mtangazaji wa TBC, David Wakati, alipofika nyumbani kwa marehemu huyo  Oysterbay jijini Dar es Salaam jana Desemba 2, kwa ajili ya kutoa mkono wa pole. Marehemu Wakati alifariki juzi jijini Dar es Salaam.

Friday, 2 December 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA BARABARA YA NELSON MANDELA TEMEKE JIJINI DAR.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKt. Mohammed Gharib Bilal na Kaimu Balozi wa Umoja wa Ulaya, Enrico Strampeli, wakifunua kitambaa kwa pamoja ikiwa ni sehemu ya Ufunguzi wa  jiwe la Msingi la Barabara, wakati wa ufunguzi wa Barabara hiyo ya Mandela uliofanyika jijini Dar es Salaam, Desemba 2.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu baada ya kufungua rasmi Barabara ya Nelson Mandela, uliofanyika Desemba 2, Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Kaimu Balozi wa Umoja wa Ulaya, Enrico Strampeli , wakikata upete kwa pamoja ikiwa ni ishara ya ufunguzi rasmi wa Barabara ya Nelson Mandela, uliofanyika leo Desemba 2, Temeke Jijini Dar es Salaam. Kulia kwa Makamu ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli na (kulia) kwa Balozi ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadick.

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WATANZANIA WAISHIO BURUNDI

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati alipokutana na Watanzania waishio nchini Burundi jana Novemba 30. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Dkt. James Mwasi Nzagi (kulia) ni Mwenyekiti wa Kinamama wa Jumuiya ya Kinamama waishio Burundi, Siwajibu Hamis (wa pili kulia) ni Mwenyekiti wa Vijana wa Jumuiya hiyo, Mutalemwa Julian.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwaaga baadhi ya Watanzania waishio Burundi baada ya kumaliza mazungumzo alipokutana nao Bujumbura Burundi jana Novemba 30 na kuzungumzia mambo mbalimbali yanayoendelea katika Taifa la Tanzania.