Friday 14 October 2011

MAKAMU WA RAISI KATIKA SHUGHULI YA KUWASHWA KWA MWENGE WA UHURU.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Mwenge wa uhuru kiongozi wa mbia za mwenge huo mwaka 2011 2012 Mtumwa Rashid Halfan kutoka mkoa wa kaskazini Unguja, kwa ajili ya kuanza mbio za kukimbiza katika mikoa yote ua Tanzania baada ya kuuwasha rasmi leo katika kijiji cha Butiama Mkoani Mara.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka shada la mauwa kwenye Kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwalim Julius Nyerere baada ya misa maalum ya kumkumbuka muasisi huyo Taifa la Tanzania iliyofanyika leo kijijini kwake Mwitongo Butiama.

No comments:

Post a Comment