Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya marehemu Profesa, Samuel Mushi, aliyefariki wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. Shughuli za maziko na kuaga mwili wa marehemu zilifanyika kwenye Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo Julai 27, 2011. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima ya mwisho mbele ya jeneza lenye mwili ya Marehemu Profesa Samuel Mushi, wakati alipofika katika shughuli ya kuaga iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leo Julai 27, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, pamoja na baadhi ya viongozi wakiwa katika shughuli ya mazishi na kuaga mwili wa marehemu Profesa Samuel Mushi, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo Julai 27, 2011.
No comments:
Post a Comment