Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,mkewe Mama Zakhia Bilal na Mama Maria Nyerere,wakiwa pamoja na baadhi ya Marais wa nchi za Afrika wakati walipohudhuria katika maadhimisho ya Kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Muasisi na Rais wa Msumbiji, Samora Machel, zilizofanyika leo Oktoba 19, mjini Maputo Msumbiji.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na aliyekuwa mke wa Rais wa zamani wa Msumbiji, Mama Grace Machel, wakati walipokutana na katika viwanja vya Mozambique Heroes Square, kwenye sherehe za maadhimisho ya Kumbukumbu ya kifo cha muasisi wa nchi hiyo, Samora Machel, zilizofanyika leo Oktoba 19, mjini Maputo. Kulia kwa Makamu ni Mama Zakhia Bilal na (katikati) ni Rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma.
No comments:
Post a Comment