Monday, 13 September 2010

Dk Bilal awaasa wasomi nchini


Lindi MGOMBEA mwenza wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Dk.Mohamed Bilal amewashauri wasomi kote nchini kuanzisha utamaduni wa kujenga makazi yaliyobora ili taifa liweze kupiga hatua katika sekta ya makazi. Kauli hiyo ya Dk Bilal aliitoa wakati akihutubia mamia ya wakazi wa Manisapaa ya Lindi ambapo pia alitumia nafasi hiyo kumnadi mgombea ubunge kupitia CCM, Mohamed Abdulaziz.“Zamani tukisoma chuo kikuu na kuhitimu hatukumudu hata kununua simu. Siku hizi kila mwananchi anayo fursa ya kupata simu. Vijana wetu siku hizi wanahitimu vyiuo vikuu na baada ya mwaka mmoja wanaweza kununua magari. Nadhani sasa ni wakati muafaka kwa wao kuanza mkakati wa kujenga makazi bora,” alisema na kuongeza; “Tunao mpango madhubuti wa kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata makazi bora. Mpango huu upo katika ilani yetu na ni imani yangu kuwa wananchi wakimchagua Rais Kikwete katika uchaguzi ujao, basi itakuwa kazi rahisi kwetu kufanikisha azma hii muhimu katika maendeleo ya wananchi wetu.” Dk Bilalbado anaendelea na kampeni katika mkoa wa Lindi ambapo jana alifanikiwa kufanya kampeni katika wilaya za Ruangwa, Liwale na Nachingwea. Katika kapmeni hizo, Dk Bilal alisisitiza umuhimu wa wananchi kutambua kuwa serikali ya CCM imejipanga vema na kwamba ina kila sababu za kutaka kuwapa maendeleo zaidi ya hapo walipo. Msomi huyu wa masuala ya Nyuklia alifafanua pia kuwa, serikali ya CCM inatambua kero za barabara zinazoikabili mikoa ya Kusini na kwamba hatua za kukabiliana na hali hiyo zinaonekana kwa kuwa barabara nyingi zinafanyiwa kazi kwa sasa.Pia alisisitiza umuhimu wa wananchi kuchangamkia fursa za Kilimo Kwanza kwa kuhakikisha kuwa wanawatumia wataalam wachache waliopo sambamba na fursa kama mbegu na mbolea zinazohamasishwa na wananchi kutolewa. Tena alifafanua kuwa, anayo taarifa ya kero kuhusu zao la Korosho na akawaeleza wananchi kwamba tiba ya kero hiyo ipo na rais Kikwete ameshafanya kila awezalo kuhakikisha vyama vya ushirika vinaimarishwa sambamba na kuwapa bei bora wakulima wa Korosho.Mgombea Mweza, Dk Bilal alifafanua pia umuhimu wa wazazi kuwajali watoto wao na kuhakikisha wanawapeleka katika shule za awali kwa kuwa ilani ya CCM inatamka wazi kuwa, ifikapo mwaka 2015, kila shule ya Msingi itatakiwa kuwa na shule hizo, hivyo wazazi wachangamkie fursa hiyo iliyopo mbele yao.Sambamba na hilo, gari mmoja lilokuwa ndani ya msafara wa mgombea huyo liliacha njia na kupinduka katika kijiji cha Nangumbo wilaya ya Ruangwa mkoani majira ya saa nne, asubuhi, wakati magari hayo yakiwa katika njia ya kwenda makao makuu ya wilaya ya Ruangwa kwa ajili ya mkutano wa kampeni.Shuhuda wetu aliyekuwepo katika tukio hilo alieleza kuwa, gari hilo lilipata ajari kufuatia vumbi kali liliolosababisha dereva wa gari kutoona mbele huku akitakiwa kupita katika eneo lililo[kuwa na tuta kubwa.Gari hilo lilikuwa na abiria wane, lakini wote walisalimika na baada ya jitihada za kuwatioa katika gari hilo kukamilika, msafara uliendelea kama kawaida.

No comments:

Post a Comment